KWA MAONI,USHAURI,HABARI NA MATANGAZO MBALIMBALI WASILIANA NASI NAMBA +255714545215(for SMS)
Saturday, September 29, 2012
RICK ROSS IN TANZANIA..................
Msanii wa hip hop kutoka Marekani Rick Ross annatarajia kufanya shoo kali katika Tamasha la Fiesta litakalo fanyika katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni,Jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi ya tarehe 06/10/2012.Msanii Rick Ross ndio mara yake ya kwanza kuja Tanzania,Anatarajiwa kusindikizwa na wasanii kibao wa hapa Tanzania katika tamasha hilo la Fiesta 2012,kama Roma,Linnah,Mwana Fa,Diamond,Barnaba,Godzillar na wasanii wengine wengi wa hapa nyumbanii.Tamasha la Fiesta huandaliwa na Clouds Fm,Mwaka huu likiwa na kauli mbiu FIESTA 2012 BHAAAAAAAAAAAAAAAAASSSSSSSSSSSSSIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII..........
WASANII WA BONGO MOVIE WANAJISHUSHIA HESHIMA WENYEWE.....
Msanii wa Bongo flava Ney Wa Mitege alizua taflani baina na yeye na wasanii wa Bongo Movie baada ya kutoa nyimbo yake inayotambulika kwa jina la "Sema nao".Katika nyimbo hiyo alidiriki kutoa maneno na kusema "Makahaba wenye viwango wapo Bongo movie" kipande hichi cha nyimbo kilizua utata mkubwa kwa baadhi ya wasanii wa Bongo movie kwani wengine walidiriki kusema amewashushia heshima.
Sasa tuje kwa wasanii wenyewe wa Bongo Movie tujiulize Je,wanajiheshimu?huto shangaa maneno ya Ney wa mitego pale utakapo ona picha za baadhi ya wadada mastar wa bongo movie wakiwa wamepiga picha wakiwa sehemu zao za ndani zinaonekana.
Msanii kama Wema Sepetu na Aunt Ezekiel ni baadhi kati ya wale ambaao wanaongoza kwa kuonekana kwa picha zao wakiwa sehemu zao za ndani zinaonekana.
Sasa jiulize wanataka heshima kweli katika jamii inayo wazunguka?je.kukaa kwao uchi kunafaida yeyote wanaopata?Je nani atakubali mtoto wake kuiga wasanii hawa kama kioo cha jamii?
Bongo Movie tunaipenda na tunaiheshimu ila kati yenu ndio mnatukosea heshima washabiki wenu.
Tuesday, September 18, 2012
PROGRAME KABAMBE YA KUSAKA VIJANA WENYE VIPAJI INAKUJA.
Mkurugenzi wa kampuni ya Solowa Art Promotion Ndugu Omari Mcheni Solowa amesema kampuni yake imeamua kutoa nafasi kwa vijana na kuamua kusaka vijana wenye vipaji vya sanaa hasa katika tasnia ya muziki na kucheza.
Aidha ndugu Omari M Solowa amesema kuwa programe hiyo ya kutafuta vipaji anategemea kuanzia Mkoa wa Tanga kisha ataendelea kuzunguka mikoa mingine kuhakikisha kila kijana mwenye kipaji na ndoto ya kuwa msanii mkubwa anamfikia,''lengo la programe hii ni kutafuta vijana wenye vipaji vya kuimba na moja kwa moja tutawachukua na kusimamia kazi zao mpaka tuhakikishe wanatimiza malengo yao''alisema Solowa.
Pia ameaomba wadau mbalimbali yajitokeze kudhamini mashindano hayo kwani kufanya hivyo ndio njia mojawapo ya kuwapatia vijana ajira kupitia vipaji vyao.
kwa yeyote atakayeataka kudhamini mashindano hayo nafasi ipo wazi,wasiliana nasi:
email:solowamimi@yahoo.com
mobile :+255 714545215
Thursday, September 13, 2012
WELCOME TANZANIA FOR TOURISM,HOSPITALITY,PEACEFULLY HERE.............
highest mountain in Africa,Mount Kilimanjaro
Waterfall in Amani, Tanga.
nice place
The Masai Tribe in Arusha,Tanzania,
Dar es salaam, Tanzania.
Have a nice beaches here.
Lake Victoria in Mwanzan Tanzania.This Lake is the source of River Nile.
Indian Ocean in Dar es salaaam,Tanzania.
Mafia Island in Tanzania.
Have nice Hotels
for futher information,email us: solowamimi@yahoo.com
MTUHUMIWA WA KIFO CHA DAVID MWANGOSI APANDISHWA KIZIMBANI.
Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha channel ten kituo cha Iringa Marehemu David Mwangosi,afande Pasificus Cleophace Simon(23) mkazi wa FFU Iringa mwenye nambari za kijeshiG2573(aliyejifunika uso) akifikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka ya mauaji.
Mnamo september 2,2012 katika kijiji cha Nyololo Mkoani Iringa,alimuua David Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i ya makosa ya jinai.
Mtuhumiwa alijifunika kofia akiwa chini ya ulinzi wa polisi wenzie.
Gari lililomleta mtuhumiwa.
Mnamo september 2,2012 katika kijiji cha Nyololo Mkoani Iringa,alimuua David Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i ya makosa ya jinai.
Mtuhumiwa alijifunika kofia akiwa chini ya ulinzi wa polisi wenzie.
Gari lililomleta mtuhumiwa.
Wednesday, September 12, 2012
BI KIDUDE,MSANII MKONGWE KULIKO WOTE HAPA TANZANIA.
Tuesday, September 11, 2012
WAANDISHI WA HABARI WAANDAMANA KUPINGA MAUUAJI YA MWENZAO.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari vya hapa Tanzania wakiandamana kuelekea viwanja vya jangwani Jijini Dar es salaam.
Kwa hisia kali wanaandamana kupinga mauaji ya kikatili yaliofanya na polisi kumuua mwandishi wa kituo cha channel 10 mkoani Iringa Ndugu Daud Mwangosi yaliotokea september 2.
Katibu mkuu wa jukwaa la wahariri Tanzania Ndg.Nevil Meena akitoa tamko katika maandamano hayo jijini Dar es salaam.
Kwa hisia kali wanaandamana kupinga mauaji ya kikatili yaliofanya na polisi kumuua mwandishi wa kituo cha channel 10 mkoani Iringa Ndugu Daud Mwangosi yaliotokea september 2.
Katibu mkuu wa jukwaa la wahariri Tanzania Ndg.Nevil Meena akitoa tamko katika maandamano hayo jijini Dar es salaam.
Monday, September 10, 2012
THOMAS MOURRIS MNKAY,MKALI ASIYE NA BAHATI YA KUITWA TIMU YA TAIFA.
Anaitwa Thomas Morris Mnkay ukimwangalia kwa makini uwanjani unaweza kukubaliana nami kwa kusema kwamba hana bahati ya kuitwa katika timu ya Taifa.Ni mtanzania ambaye kwa sasa anacheza katika timu ya Bandari ya Mombasa Kenya..Thomas Morris ambaye alishawahi kuchezea timu kubwa maarufu hapa Tanzania kama Kariakoo Lindi,Miembeni,Yanga African na Mtibwa sugar ambazo zote zinashiriki na zilishiriki ligi kuu ya hapa Tanzania.Katika historia fupi ya soka Thomas Morris alishacheza mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa,Aliingoza Yanga SC katika mashindano ya klabu bingwa Africa mwaka 2006-2007.Thomas Morris alikua mmoja kati ya wachezaji waliokuwa wanafunga magoli mengi katika ligi kuu ya Tanzania na mashindano mbalimbali.tt
Add caption |
TUME YA KATIBA INAENDELEA NA MAJUKUMU YAKE NA SASA IPO MKOANI RUVUMA.
Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Sinde Warioba akizunguamza na waandishi wa habari katika hoteli ya Seed Farm Villa mjini Songea jana kuhusu ukusunyaji wa maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya,kulia ni kiongozi wa timu hiyo inayokusanya maoni mkoani Ruvuma Profesa Mwesiga Baregu.