KWA MAONI,USHAURI,HABARI NA MATANGAZO MBALIMBALI WASILIANA NASI NAMBA +255714545215(for SMS)
Tuesday, September 18, 2012
PROGRAME KABAMBE YA KUSAKA VIJANA WENYE VIPAJI INAKUJA.
Mkurugenzi wa kampuni ya Solowa Art Promotion Ndugu Omari Mcheni Solowa amesema kampuni yake imeamua kutoa nafasi kwa vijana na kuamua kusaka vijana wenye vipaji vya sanaa hasa katika tasnia ya muziki na kucheza.
Aidha ndugu Omari M Solowa amesema kuwa programe hiyo ya kutafuta vipaji anategemea kuanzia Mkoa wa Tanga kisha ataendelea kuzunguka mikoa mingine kuhakikisha kila kijana mwenye kipaji na ndoto ya kuwa msanii mkubwa anamfikia,''lengo la programe hii ni kutafuta vijana wenye vipaji vya kuimba na moja kwa moja tutawachukua na kusimamia kazi zao mpaka tuhakikishe wanatimiza malengo yao''alisema Solowa.
Pia ameaomba wadau mbalimbali yajitokeze kudhamini mashindano hayo kwani kufanya hivyo ndio njia mojawapo ya kuwapatia vijana ajira kupitia vipaji vyao.
kwa yeyote atakayeataka kudhamini mashindano hayo nafasi ipo wazi,wasiliana nasi:
email:solowamimi@yahoo.com
mobile :+255 714545215
No comments:
Post a Comment