www.nipetanosolowa.blospot.com

Saturday, September 29, 2012

WASANII WA BONGO MOVIE WANAJISHUSHIA HESHIMA WENYEWE.....


 Msanii wa Bongo flava Ney Wa Mitege alizua taflani baina na yeye na wasanii wa Bongo Movie baada ya kutoa nyimbo yake inayotambulika kwa jina la "Sema nao".Katika nyimbo hiyo alidiriki kutoa maneno na kusema "Makahaba wenye viwango wapo Bongo movie" kipande hichi cha nyimbo kilizua utata mkubwa kwa baadhi ya wasanii wa Bongo movie kwani wengine walidiriki kusema amewashushia heshima.
    Sasa tuje kwa wasanii wenyewe wa Bongo Movie tujiulize Je,wanajiheshimu?huto shangaa maneno ya Ney wa mitego pale utakapo ona picha za baadhi ya wadada mastar wa bongo movie wakiwa wamepiga picha wakiwa sehemu zao za ndani zinaonekana.
   Msanii kama Wema Sepetu na Aunt Ezekiel ni baadhi kati ya wale ambaao wanaongoza kwa kuonekana kwa picha zao wakiwa sehemu zao za ndani zinaonekana.
    Sasa jiulize wanataka heshima kweli katika jamii inayo wazunguka?je.kukaa kwao uchi kunafaida yeyote wanaopata?Je nani atakubali mtoto wake kuiga wasanii hawa kama kioo cha jamii?
Bongo Movie tunaipenda na tunaiheshimu ila kati yenu ndio mnatukosea heshima washabiki wenu.

No comments: