www.nipetanosolowa.blospot.com

Tuesday, July 31, 2012

TANZANIA NA MALAWI ZAKUTANA KUJADILI MGOGORO WA MPAKA.

      Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Mhe.Benard Membe(kushoto) na waziri wa mambo ya nje wa Malawi Mhe. Epraim Chiume wakipata chai kabla ya kikao cha kuhusu mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi katika hotel ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam hivi karibuni.
      Balozi wa Tanzania nchini Malawi Patrick Tsere na balozi wa malawi hapa nchini Bibi Flossie Chidyaonga wakiwasalimiana kwa furaha walipokutana katika mkutano huo kuhusu mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi.
    Baadhi ya maofisa wa timu ya Tanzania katika majadiliano hayo wakiwa wanasubiri kuingia katika kikao hicho.

KUTOKANA NA MGOMO WA WALIMU UNAOENDELEA NCHINI,MKOA WA DODOMA WAMETOA TAMKO LAO JUU YA MGOMO HUO.

 Moja ya shule iliyo athilikika na mgomo wa walimu wanafunzi wakiwa wanazurura nje sababu walimu wao hawakuingia madarasani kufundisha,hii inatokana na sababu ya mgomo uliotangazwa na chama cha waalimu taifa.
    Mgomo huu umekuja kipindi  ambacho wanafunzi wa darasa la saba wanajiandaa na mtihani wao wa kumaliza elimu ya msingi.

Monday, July 30, 2012

WALIONGOZA KWA MAGOLI CECAFA KAGAME CAP 2012.




PATA VICHWA VYA HABARI VYA BAADHI YA MAGAZETI YA HAPA NCHINI.

























BONDIA MTANZANIA SELEMANI KIDUNDA APOTEZA MCHEZO WAKE WA KWANZA KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI LONDON.

        Wadau wa michezo walioko London,kushoto Ndg. Amosi Msanjila afisa wa ubalozi London,mtangazaji maarufu wa BBC Ndg. Charles Hilary,makamu wa rais TBF Ndg. Phares Magesa na mchambuzi mahiri wa michezo wa BBC Ndg. Israel Saria.
     Bondia wa Tanzania Selemani Kidunda mwenye fulana nyekundu akiwa na viongozi na baadhi ya wadau wa michezo wakati akienda kupigana bondia toka Moldova Belous Vasilii,Kidunda alipoteza mchezo huo kwa point 7-20.

watch the video

Roma mkatolika ndani ya coco beach live show.

Sunday, July 29, 2012

Rais Kikwete afungua kongamano la tatu la jikwaa la uhusiano wa China na Africa katika kupunguza umasikini.

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kongamano la tatu la jukwaa la uhusiano wa China na Bara la Afrika lenye lengo la kuondoa umasikini katika hotel ya White Sands iliyopo jijini Dar es salaam july 28,2012.
    Wa tatu kutoka kushoto ni waziri wa wa China anayeshughulikia umasikini Mhe.Fan Xiaojian,wa pili kulia na waziri wa ofisi ya rais Mhe. Steven Wassira,wa pili kushoto ni naibu waziri wa fedha na maendeleo Sierra Leone Mhe. Momodu Kargbo,kushoto ni katibu mtendaji wa tume ya mipango Dkt. Philip Mpango na kulia kabisa na balozi wa China hapa nchini Mhe. L.V.Youqing.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ufunguzi wa kongamano la tatu la jukwaa la uhusiano wa China na Bara la Afrika katika hotel ya White Sands jijini Dar es salaam july 28,2012.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza waziri wa china anayeshughulikia umasikini Mhe. Fan Xiaojian(kushoto) na balozi wa China hapa nchini Mhe. L.V.Youqing baada ya kufungua kongamano la tatu la jukwaa la uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umasikini.

WABUNGE WANAPATA FUTARI YA PAMOJA.

 Wabunge wakifuturu kwenye ukumbi wa basement,bungeni mjini Dodoma julai 28,2012.Futari hiyo imeandaliwa na wabunge waislamu na waliofuturu ni wabunge wa dini zote pamoja na madereva wa wabunge.
Baadhi ya wabunge walioudhuria futari katika ukumbi wa basement,bungeni mjini Dodoma julai 28,2012.

Saturday, July 28, 2012

YANGA BINGWA KAGAME CUP 2012

Hatimaye kila chenye mwanzo kina mwisho,huo ni usemi wa kale uliodhihirika baada ya kuwa na tambo mbalimbali kuhusiana na timu zilizoingia fainal ya cecafa kagame cup 2012 kati ya Azam FC na YANGA SC,tambo hizo zimekuja baada ya kuonekana kuwa Azam FC imekuwa tishio kwa timu kongwe hapa nchini,Azam FC ilifanikiwa kuion
dosha SIMBA SC katika mashindano hayo na kutinga nusu fainali kwa kishindo hatimaye fainali na kukutana na timu kongwe nyingine hapa nchi YANGA SC,Watuwengi walionekana kulizungumzia sana pambano hilo la fainali na kuamini fainali itakuwa ya pekee kama ilivyokuwa.

 Kikosi cha Yanga lilichotwaa ubingwa Kagame Cup 2012 yaliofanyika jijini Dar es salaam.
 Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh, Said Meck Sadick akikagua timu katika mchezo wa fainal kati ya Yanga na Azam FC leo,
 mkuu wa mkoa akikagua timu ya Azam FC katika mchezo wa fainali kati yao na Yanga,Azam walikubali kipigo cha mabao 2-1.
 Mfungaji wa bao la kwanza kwa mabingwa wa Kagame Cup 2012 Yanga SC Hamis Kiiza akimtoka beki wa Azam FC Jabir Azizi katika mchezo huo wa fainal.
 Mchezaji wa Yanga aliyefanya vizuri katika mashindano hayo ya Kagame Cup 2012 Said Bahanuz akimtoka beki wa Azam FC Aggrey Morris katika mchezo huo wa fainal ya Kagame Cup 2012.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na mchezaji Hamis Kiiza katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Add caption
Mabungwa wa Cecafa Kagame Cup 2012 Yanga SC ya Tanzania,wakishangilia baada ya kutawadhwa mabingwa wa mashindano hayo.Yanga walifanikiwa kunyakuwa ubingwa baada ya kuifunga Azam FC kwa jumla ya mabao 2-1.

Fainal Kagame Cup inaendelea,,,Dk 64,YANGA 1-0 AZAM



mambo yanavyoendelea katika uwanja wa taifa,washabiki wa Yanga na Azam FC wakifatilia mechi ya fainali kwa makini,
dakika ya 64 Yanga FC wanaongoza kwa goli moja lililofungwa na mchezaja Hamisi Kiiza.