www.nipetanosolowa.blospot.com

Saturday, July 28, 2012

YANGA BINGWA KAGAME CUP 2012

Hatimaye kila chenye mwanzo kina mwisho,huo ni usemi wa kale uliodhihirika baada ya kuwa na tambo mbalimbali kuhusiana na timu zilizoingia fainal ya cecafa kagame cup 2012 kati ya Azam FC na YANGA SC,tambo hizo zimekuja baada ya kuonekana kuwa Azam FC imekuwa tishio kwa timu kongwe hapa nchini,Azam FC ilifanikiwa kuion
dosha SIMBA SC katika mashindano hayo na kutinga nusu fainali kwa kishindo hatimaye fainali na kukutana na timu kongwe nyingine hapa nchi YANGA SC,Watuwengi walionekana kulizungumzia sana pambano hilo la fainali na kuamini fainali itakuwa ya pekee kama ilivyokuwa.

 Kikosi cha Yanga lilichotwaa ubingwa Kagame Cup 2012 yaliofanyika jijini Dar es salaam.
 Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh, Said Meck Sadick akikagua timu katika mchezo wa fainal kati ya Yanga na Azam FC leo,
 mkuu wa mkoa akikagua timu ya Azam FC katika mchezo wa fainali kati yao na Yanga,Azam walikubali kipigo cha mabao 2-1.
 Mfungaji wa bao la kwanza kwa mabingwa wa Kagame Cup 2012 Yanga SC Hamis Kiiza akimtoka beki wa Azam FC Jabir Azizi katika mchezo huo wa fainal.
 Mchezaji wa Yanga aliyefanya vizuri katika mashindano hayo ya Kagame Cup 2012 Said Bahanuz akimtoka beki wa Azam FC Aggrey Morris katika mchezo huo wa fainal ya Kagame Cup 2012.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na mchezaji Hamis Kiiza katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Add caption
Mabungwa wa Cecafa Kagame Cup 2012 Yanga SC ya Tanzania,wakishangilia baada ya kutawadhwa mabingwa wa mashindano hayo.Yanga walifanikiwa kunyakuwa ubingwa baada ya kuifunga Azam FC kwa jumla ya mabao 2-1.

No comments: