Msanii kutoka Tanga Dr leader aliyetamba na nyimbo kama "Msambaa" iliomtambulisha ambayo aliifanya chini ya mtaarishaji wa mziki marehemu Mr Ebbo,na kufanya vizuri katika anga za miduara na nyimbo kama "Macho kodo ft Dr John" na "Mbuzi kagoma" na nyingine nyingi.
Dr leader amenihabarisha kwamba sasa yupo mbioni kuandaa project zake baada kuingia mkataba mnono na meneja ambaye alisema ni mapema kumtaja"najiandaa kwa project zangu ambazo naamini ndio itakuwa ujio wangu baada ya kuwa kimya,sasa najiandaa kufanya video ya nyimbo yangu Mbuzi kagoma kwenda na Raha ya pwani".alisema Dr leader
Dr leader anatambulika katika tasnia ya muziki kwa kuchanganya nyimbo zake na lugha ya kisambaa.
No comments:
Post a Comment