www.nipetanosolowa.blospot.com

Friday, August 3, 2012

RAIS ATOA NG'OMBE 1500 MKOANI ARUSHA KAMA KIFUTA JASHO.

              Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kwa kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu mkoani Arusha(Longido,Monduli na Ngorongoro).Kulia kwake ni mbunge wa jimbo la Monduli Mhe. Edward Lowassa na kushoto kwake ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu(sera na uratibu bunge)Mhe. William Lukuvi.
         Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa kijiji cha Makuyuni wilayani Monduli alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng,ombe 1500 kila mwezi kwa wilaya tatu za Arusha.
        Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi ng'ombe mmoja wa wakaazi wa Monduli.
        Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli Mhe. Edward Lowassa wakiteta jambo baada ya kufanyika mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wilaya tatu mkoa wa Arusha.Rais alitoa ng'ombe kama kifuta jasho kwa wananchi baada ya kupoteza ng'ombe 800,000 kutokana na athari za ukame uliotokea mwaka 2008/2009.

No comments: