www.nipetanosolowa.blospot.com

Saturday, August 11, 2012

KAZI FEKI ZA WASANII WA BONGO ZAKAMATWA.

Mkurugenzi wa kampuni ya msama promotion Mr Alex Msama naendeleza harakati za kuhakikisha wasanii wa Tanzania angalau wanafaidika na kazi zao baada ya kufanikisha kukamatwa kwa kopi feki za kazi za wasanii wa hapa nchini,Hapa Tanzania wasanii hawanufaiki na kazi zao,hii ni kutokana na wizi uliokithiri wa kazi zao,harakati alizo kuwa nazo Mr Msama kwa kushirikiana na jeshi la polisi inaonekana kupunguza makali ya wizi wa kazi za wasanii hapa nchini huku wakiwa wanasubiri kupitishwa kwa sheria ya hati miliki ambayo ndio kilio cha wasanii hapa nchini,Pia mdau wa sanaa hapa nchini unashauriwa kuto nunua kazi ambayo ni feki kwani hufanya wasanii wetu kuto nufaika na kufanya kupunguza kasi ya maendeleo.Kwakweli inasikitisha sana kuona msanii anaandaa kazi kwa mamilioni ya pesa kisha unakuta kazi feki inayouzwa tena mpaka shilingi elfu moja,huu ni unyonyaji mkubwa ambao tunatakiwa kuupinga vikali kwa kununua nakala ya kazi ya msanii original.


No comments: