www.nipetanosolowa.blospot.com

Wednesday, August 1, 2012

HII NI HOJA YANGU BINAFSI.....

                      TUJADILI KATIBA IJAYO IWEJE?.

   Nimeamua kutoa hoja hii tusaidiane kuchangia mawazo na Watanzania wenzangu hasa katika kipindi hichi cha mchakato wa kuandaa katiba mpya.Mambo mengi yanayoendelea katoka bunge letu la jamuhuri ya muungano wa Tanzania yamenifanya nitambue mambo kadhaa ambayo tunaitaji kuyarekebisha katika katiba yetu mpya ijayo kama Mhe Rais wetu alivyotuahidi.
  Kutokana na migomo mingi inayotokea hapa nchini na kashfa tunazozisikia kila siku bungeni mimi naona sasa ni wakati wa kurekebisha sheria zetu kwa manufaa yetu watanzania hasa tusiokuwa na sauti.Kila siku tunasikia juu ya ubadhilifu wa pesa kwa baadhi ya vingozi na maafisa wa serikali lakini cha ajabu ni mara chache kusikia wkipelekwa mahakamani na hata wakipelekwa hatma za kesi zao hazijulikani zinakwenda vipi.
Pia ni wakati wa kutengeneza sheria itakayo ifanya Bunge kujadili masuala muhimu hata kama yatakuwa yashapelekwa mahakamani,sheria iliopo sasa kwa upeo wangu naiona ibadilishwe kwani kuna mambo mengine yanihitaji yapatiwe ufumbuzi mapema kwahiyo nafikiri kuwe na sheria itakayokuwa inaipa mamlaka bunge kujadili mambo ya dharura kama vile ule mgomo wa madaktari na huu wa walimu kwani kwa sasa bunge linashindwa kujadili sababu tayari lipo mahakamani.

       Wewe pia mfatiliaji wa blog hii unaweza kutoa maoni yako kwa kucomment na hata kama unazaidi ya hichi we eleza tu na tuone Watanzania kipi wanahitaji.

No comments: