www.nipetanosolowa.blospot.com

Wednesday, August 1, 2012

CHUJI,BAHANUZI NA RIDONDO WAITWA TAIFA STARS.

                                                     Kocha wa Taifa Stars Kim Poulsen.

    Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen amewaita katika kikosi hicho wachezaji Athumani Iddy Chuji,Said Bahanuzi na Ramadhani Chombo Ridondo katika kikosi cha wachezaji 21,Taifa Stars wanajiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa Agosti 15,
     Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati anatangaza kikosi hicho,kocha Kim amesema wachezaji hao wameonyesha umahili mkubwa katika KOMBE LA KAGAME .
   Kocha Kim Poulsen amewatema wachezaji chipukizi Edward Christopher,Jonas Mkunde na Juma Nyoso wote wa Simba,Nurdin Bakari wa Yanga na  Waziri Salum wa Azam FC.
   Timu hiyo itaingia kambini Agosti Nane kuanza mazoezi kabla ya kuondoka Agosti 14 kwenda kucheza na timu itakayo thibitisha kucheza nz Stars ugenini wakati wowote kuanzia sasa.

No comments: