www.nipetanosolowa.blospot.com

Friday, August 3, 2012

LISA JENSEN AFANYA VIZURI MISS WORLD.

      Mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Miss World Lisa Jensen ameanza kufanya vizuri katika michuano hiyo baada ya kufanikiwa kuingia kumi bora ya shindano la Top Model,hivyo kumuongezea point zaidi kabla ya fainali za kunyang'anyiro hicho.
    Habari kutoka Momgalia ambako shindano la Miss World litakapofanyika zinasema Lisa Jensen uwezo wake mkubwa huku akionesha kipaji cha aina yake katika shindano hilo lililofanyika majuzi usiku nchini humo.Lisa ni mmoja wa wawakilishi wa tatu wa Bara la Afrika ambao wamefanikiwa kupenya na kuingia katika nafasi hiyo muhimu.
    Waafrika wengine waliofanikiwa kupenya katika kumi bora ya shindano hilo kabla ya siku ya fainali ya Miss World Agost 18,2012 ni mrembo wa Afrika Kusini na Washelisheli.
    Lisa Jensen amefanikiwa kufanya kweli na kuwatoa kimasomaso Watanzania ambao kwa sasa wanajikuta katika hali mbaya kutokana na wanamichezo wake waliopo katika michuano ya olimpiki kufanya vibaya.Kutokana na kuingia kumi bora Lisa bado ana kazi kubwa ya kuhakikisha anapambana ndani ya wiki hii wakati mshindi wa Top Model atakaposakwa rasmi.

2 comments:

baja said...

lisa jensen kwan ndo miss bongo?

Anonymous said...

yap baja...alichaguliwa kwa ajili ya kuwakilisha Tanzania katika shindano dogo la kumsaka mwakilishi.